RUBY AMCHANA LIVE DIVA WA CLOUDS.

Muimbaji wa ‘Na Yule’ Ruby amefunguka baada ya mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva kudai kuwa hamfahamu msanii huyo.Ruby ameiambia Bongo5 kuwa kauli aliyoitoa mtangazaji huyo anaiona ni kama utoto. “Naona ni ujinga, I don’t want to talk about it, naona ni utoto sidhani kama ninaweza kuliongelea hilo.”“Everybody knows me, so nahisi huo ni utoto tu labda wa kukosa majibu kwenye maswali ya interview aliyohojiwa. I don’t to talk about her,” ameongeza.Pia Ruby amedai kuwa licha ya kuzinguana na uongozi wa THT, bado mambo yanaenda mswano.
“Kutokuwa na mawasiliano mazuri na uongozi wangu wa zamani sijaathirika kwakweli, sitaki kuliongelea hilo kwa sababu mimi naona kwangu ni kitu ambacho kimeshapita nataka niongelee vitu ambavyo vinaendelea mbele. Sidhani kama nina tofauti na wao mimi sijui ila, I don’t talk about them, at all.”Inawezekana Diva alitoa kauli hiyo kutokana na Ruby kutokuwa na mawasiliano mazuri na Clouds Media baada ya kushindwa kuhudhuria kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika Mwanza, August 20 ya mwaka huu.

Story by:@Joplus_

Source: Raha za walimwengu