DIAMOND ATENGA 25% YA MAPATO YA WIMBO WAKE WA “SALOME” NA KUZIELEKEZA KWA SAIDA KAROLI.

Hivi unafahamu kuwa 25% ya mapato ya ngoma ya “Salome” ambayo imeachiwa juzi na Diamond Platnumz yataenda kwa mwanadada Saida Karoli?.

Kama ulikuwa hujainyaka hiyo basi ichukue, ni exclisive imetoka kwa Diamond Platnumz. Mkali huyo ameamua kufanya hivyo kama kulipa fadhila kwa mwanadada Saida karoli na uongozi wake mzima kwa kumpa ruhusa na baraka zote kwa kuurudia wimbo huo, ukiangalia ni wimbo ambao umepata mafanikio makubwa sana kwa muda mfupi.

Akiongea na Perfect255 Diamond Platnumz ameweka wazi ni jinsi gani alivyo na mapenzi na wimbo huo hadi kufikia hatua ya kuurudia.

Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo yameongelewa na Diamond Platnumz kuhusu ngoma ya Maria Salome. Itazame video hii hapa chini kusikiliza interview nzima na kujua ilikuaje hadi akaingia studio, na kwanini ilikuwa Raymond na si mwingine.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com