RAYMOND A.K.A RAYVVANY WA WCB AMESEMA YEYE HARINGI WALA HANA DHARAU BALI ANAFUATA MISINGI YA KAZI.

Msanii wa WCB, Raymond, amedai kuwa wakati mwingine anapofuata sana misingi ya kazi, baadhi ya watu hudhani kuwa anaringa, kitu ambacho anadai hawezi kuwa nacho.

“Kwa mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha, aniombe namba ya simu,” Ray alimweleza Prince Ramalove wa Kings FM.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.
“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi sababu ndio unaonipa hela,” aliongeza.
Story by:@Joplus_
Source: Udaku Special Blog