SAFAREE AMTUPIA LAWAMA MEEK MILL KUWA NDO CHANZO CHA YEYE KUACHANA NA NICKI MINAJ.

Mpenzi wa zamani wa Nick Minaj, Safaree ameibuka tena na safaree amemtaja Meek Mill kama chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wake na mrembo huyo uliodumu kwa miaka 12.

Safaree alidai tu kuwa Meek Mill alikuwa na mchango mkubwa wa kuharibika kwa uhusiano wake na Meek Mill bila kuweka wazi vipi, hata hivyo The Game kwenye disstrack yake “Pest Control,” anadai kuwa Meek Mill alimchongea Safaree kwa Nick kuwa anachepuka.

Pia Safaree amesema kuwa ameamua kufuta mashitaka aliyokuwa amemfungulia Nick Minaj mwanzoni kwa madai kushiriki kwenye uaandaji wa album ya mpenzi wake huyo wa zamani.

“I had started a process, and then I just was like ‘You know what? It is what it is,If you want to deal with it like that, go ahead. I ain’t tripping.’ I’m doing a lot, and I don’t want to be having to deal with depositions and courts and all of that.” Safaree Alifunguka.

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com