Profesa Jay na Rama Dee wanaukubali muziki wa Singeli hadi kuwashirikisha nyota wa muziki huo kwenye nyimbo zao, lakini si kwa mnyama TID.
Muimbaji huyo wa Confidence, ameonekana
kumkazia staa wa muziki wa Singeli, Man Fongo, baada ya kuulizwa kama anaweza kufanya wimbo naye.
Akiongea na kipindi cha Friday Night Live cha EATV, muimbaji huyo amesema kwa sasa
haitawezekana, labda mwaka 2020.
“Nitakuwa tayari mwaka 2020 na si sasa, pamoja na kwamba utakuwa mwaka wa uchaguzi lakini ndiyo kitakuwa kipindi kizuri cha kufanya hivyo lakini kwa sasa hivi sipo tayari nina kazi nyingi nazifanya,” alisema TID.
Kwa sasa muziki wa Singeli umeonekana
kukubalika zaidi na unatabiriwa kutengeneza nyota wengi zaidi katika miaka inayokuja.
Story by:@Joplus_
Source: Perfect255.com