SINGELI YAMFANYA AFANDE SELE KUMTOA PROFESOR JAY KWENYE LIST YA WANA HIP HOP.

Mwezi wa 7 mwaka huu msanii mkongwe wa Hiphop nchini Tanzania Professor Jay aliwa-suprise mashabiki zake kwa kuachia ngoma ya “Kazi Kazi”, ngoma ambayo ina miondoko tofauti kabisa na aliyokuwa akifanya Professor jay hapo awali.

Ngoma ambayo ilizua gumzo kubwa mtaani hadi kumuhusisha Professor Jay kukiuka misingi ya Hiphop. Lakini alipoulizwa alidai kuwa ile aliyofanya sio Singeli bali ni Hiphop Singeli.

Kitu ambacho kiliwatoa mapovu wanamuziki wengi ambao wanafanya Hiphop na kudai kuwa hakuna muziki ambao unaitwa Hiphop Singeli bali Professor jay anatafuta tu njia ya kujitetea ili aonekane hajaondoka kwenye misingi ya Hiphop.

Mmoja kati ya wasanii ambao walisikika wakiongea juu ya hilo ni mkongwe Afande Sele, na alidai kuwa Professor Jay sio mwana Hiphop tena bali ni mwanasiasa. Ndipo kipaza cha Perfect255 kikawashwa kufanya interview na Afande Sele ili afunguke zaidi ni kwanini amesema Professor jay sio mwanahiphop tena na ni mwanasiasa.

“Professor Jay ni mwanasiasa, mjanja, mwerevu, mwanasiasa anatakiwa awe vile. Jay amesoma alama za nyakati, amefanya kitu ambacho wananchi wake wa Mikumi ambao wamempa kura wanapenda. lakini kisanii kuna watu amewakwaza, kwasababu bahati mbaya Hiphop haiishii kwenye muziki tu, hiphop ni utamaduni, kuanzia mavazi, maongezi na kila kitu. Lakini aina ya muziki ambao kafanya ni muziki flani ambao una upotoshaji kwa maadaili ya hiphop, mambo kama kuserebuka, kumwaga razi na vitu kama hivyo. Hicho ndio kimewakwaza watu wa hiphop. Lakini kwangu mimi namchukulia kama mwanasiasa na amefanya kitu ambacho siasa inamtaka kufanya. Na Jay sasa hivi tumtazame kama mwanasiasa na sio mwanahiphop, tukisema ni mwanahiphop tutakuwa tunamkosea sana.”

Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo King Afande Sele alifunguka kipindi akifanyiwa interview na Perfect255. Interview nzima nimekuwekea hapa chini kwenye hii video unaweza kuitazama.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com