LADY GAGA ATOKEA NA VALI LA KIPEKEE KWENYE ONYESHO LA MAVAZI HUKO MAREKANI.

 Mwanamuziki anaeongoza kwa vimbwanga nchini Marekani, Lady Gaga, ametokelezea akiwa ndani ya kijivazi cheusi chenye kumuonesha maumbile yake katika maonesho ya mavazi yaliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini New York nchini Marekani.

Gaga ameonekana kuvutiwa na maonesho hayo ambayo ndio aina ya mitindo ya nguo aipendayo maarufu kama GURU, Yakiwa yamevaliwa na wanamitindo maarufu wakiwemo Brandon Maxwell na Camilla kutoka New York nchini Marekani.

Lady Gaga amekua akijihusisha na masuala ya uigizaji hasa katika filamu za luninga ikiwemo “American horror story season 5” iliyofanya vizuri mwaka 2015-2016 na kumuwezesha kushinda tuzo za Oscars kama muigizaji bora wa kike.

Aidha alipozungumza na moja ya majarida ya mitindo jijini New York, Gaga amesema kwamba, amekua akivutiwa na masuala ya mitindo ya mavazi kutokana na dada yake ambae ndie mbunifu mkubwa wa nguo zake, lakini yeye anapendelea kuigiza filamu na kufanya muziki kwaajili ya mashabiki wake.

“Dada yangu ana penda sana mitindo hivyo ananifanya na mimi kuvutiwa na mitindo lakini mimi napendelea zaidi kuigiza na muziki naufanya kwasababu ndio ulitangulia katika vitu nilivyokuwa nafanya na kufanikiwa” amesema Lady Gaga.

Source:Muungwana Blog.