Staa wa muziki wa Marekani, Trey Songz ataungana na wasanii wa Afrika kwenye msimu wa nne wa kipindi cha Coke Studio Afrika 2016.
Coke Studio huwa wana utaratibu wa kuleta msanii wa kimataifa mmoja kila msimu, miaka iliyopita waliwaleta Wyclef Jean na Neyo.
“BREAKING NEWS: Joining Coke Studio Africa Season 4 is singer, songwriter, record producer and actor…@treysongz! Follow the conversation on#CokeStudioAfrica“ Coke studio wameandika kwenye mtandao wa Instagram.
Wasanii wa Tanzania ambao wanashiriki kwenye msimu huo wa nne ni Pamoja na Vanessa Mdee, Joh Makini, Yamoto Band na Diamond ambaye ameshiriki Coke studio ya Afrika kusini.
Story by:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.