Leo naomba nikusogezee Exclusive TOP 5 ya mishara yao ya kwanza ya mastaa wa soka, katika TOP 5 hii yupo Mbwana Samatta anyechezea KRC Genk ya Ubelgiji, Elias Maguli anayeichezea Dhofar FC ya Oman, Simon Msuva anayeichezea Yanga, Himid Mao wa Azam FC na staa wa soka pekee wa Ligi Kuu Tanzania bara aliyewahi kucheza World Cup na AFCON Vincent Bossou anayeichezea Yanga/Togo.
”Katika soka inatakiwa uwaze kutengeneza au kujenga jina lako kwanza kabla ya kufikiria namna ya kupata pesa, mara ya kwanza nasaini mkataba wangu wa kwanza sikuwa nafikiria sana hela nililipwa dola 100 ni hela ndogo ambayo nilikuwa naweza kununua viatu na nilikuwa nikikaa nyumbani kwa wazazi” >>> Bossou
Source: Millard ayo