Amber Lulu Akimbiwa Na Mpenzi Wake Hotelini.


MSANII na mnenguaji wa kwenye video za wasanii (video vixen) Amber Lulu, ambaye anatamba na wimbo wake wa Only You amefunguka kuhusu kukimbiwa hotelini na aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza tangu anafika Dar es salaam, mwigizaji Rammy Galis, bila sababu.

Alipoulizwa juu ya stori hiyo, Amber Lulu alifunguka na kusema:
“Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa Rammy Galis kipindi nafika Dar, tulikubaliana vizuri na Rammy tukaenda hotelini tukaagiza vyakula tukala na mambo mengine yakaendelea. Baadaye akaniambia nakuja, nikamwambia poa lakini mwisho wa siku sikumuona. Nikawa napiga simu yake mara asipokee na akipokea basi akawa ananiambia nisubiri kidogo. Sikujua kwa nini alikuwa anafanya hivyo.”

Aliongeza kwamba: “Alinipokea mizigo vizuri tukaingia hotelini baada ya hapo ndo akafanya alivyoamua kufanya, basi mimi nikampigia dad’angu simu nikamuelezea akaniambia hayo ni mambo ya kawaida basi dada akanitumia pesa nikalipia kila kitu. Baada ya hapo nikarudi zangu nyumbani na sikuwahi kuwasiliana naye tena tangu siku hiyo. “

Amber ni mwanamke asiyeishiwa kiki na skendo mjini lakini hajalikitu, anaangalia maisha yake tu. Ni msichana ambaye haogopi kufunguka mambo yanayohusiana na mahusiano yake. Haogopi kiki bali anazipenda kiki.

Source: Udaku.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!