Rais Magufuli: Makonda wewe chapa kazi, hata mimi ninasemwa kwenye mitandao


Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi.

Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa vikali.

Akizungumza Jumatatu hii kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa barabara za juu (Flyovers) Ubungo, Dar, Rais Magufuli amesema, “Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Rais amesema Watanzania wanapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

“Tumepoteza direction tumeanza kujadili personalities,”

Source:Teentz