Wolper ataja vitu vitatu vilivyomvutia kwa Harmonize

Jacqueline Wolper amevitaja vitu vitatu ambavyo vimemvutia kuwa na mahusiano na mkali wa Bongo Fleva, Harmonize.

“Upole, Ukarimu na anapenda dini na anaijua dini kabisa. Mimi naamini asingekuwa mwanamuziki angekuwa maalimu fulani hivi,” Wolper alifunguka kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Wakati huo huo Harmonize kwa sasa ameachia wimbo mpya ‘Niambie’ ambao amemuimbia mpenzi wake Wolper.

                                                              Source:Teentz