Ed Sheeran apata ajali.

Ben Watts

Pop star Ed sheeran amepata ajali ya baiskeli iliyopelekea kuvinjika kwa mkono wake wa kulia, hii inaweza kuathiri ziara yake ya muziki.

“Nimepata ajali ndogo ya baiskeli” Ed Sheeran ameandika kwenye Instagram yake “Kwasasa napata ushauri wa madaktari, hii inaweza kuathiri baadhi ya show zangu”

 

Ed sheran alikua kwenye mapumziko ya ziara yake ya dunia ya muziki ambayo ilitakiwa kuendelea wiki ijayo kwenye mji wa Taipei. Ed sheeran bado ana sho 14 kwa mwaka huu kwenye ziara yake hiyo kubwa ya kuipromote album yake ya Divide.

Source: Team tz

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!