Quick Racka Afuata Nyayo Za 2 Face Idibia.

Rapa na mkali wa kuswitch flows na mmiliki wa lebo ya muziki ya Switch Records(SwitchMusicGroup) Quick Rockar amelifanyika kazi suala lake la kufanya mabadiliko ya jina lake na kuanza kutambulika kwa msahabiki kama Switcher Baba.

Mabadiliko haya yameanza kutumika pia katika ujio wa ngoma yake mpya ‘Tosamaganga’ ambayo amemshirikisha mtayarishaji wa muziki S2kizzy ikiwa imepikwa katika jiko la Switcher Studio.

Uthibitisho wa hili, Quick alifunguka zaidi kupitia show ya XXL ya Clouds Fm akisema “Nimekuwa nikilitumia jina hili (Quick Rocka) kwa muda mrefu, nafikiri ni muda sahihi wa kubadilisha. Ni kutokana kukua pia nimebadilika vitu vingi sana, so kuanzia LEO nitakua nikijiita SWITCHER BABA lakini Rocka itakuwepo kwa chini pale kwa watu wa Instagram…”

Hata hivyo Quick anaingia katika aina ya ubadilishaji wa jina kama alivyofanya staa wa muziki kutoka Nigeria 2Face Idibia aliyebaidlisha jina kutoka katika utambulisho wake wa awali na kuanza kutumia jina la 2Baba ambalo analitumia katika muziki wake mpaka sasa.

Source: Dizzim Online.