Baada kifo cha Faru John, kuna habari hizi za Faru Fausta

 Tume maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha Faru John ilikabidhi ripoti kwa Waziri Mkuu ikisema kuwa faru huyo alikufa baada ya kukosa matibabu.

 Nakusogezea stori inayomuhusu faru mwingine anayeitwa Faru Fausta ambaye anatajwa kuwa Faru mwenye umri mkubwa zaidi Duniani anayepatikana kwenye Hifadhi ya Taifa Ngorongoro akikadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 65.

Source: Millard ayo