UTAFITI: Tatizo wanaloweza kupata watumiaji wa mitandao ya kijamii

Kukuwa kwa teknolojia hasa ya simu kumesaidia kurahisisha maisha ya watu wengi ambao wanakiri hawawezi kuishi bila Smartphones, leo March 29 2017 millardayo.com imekutana na stori inayohusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika maisha ya kila siku husababisha msongo wa mawazo kwa mujibu wa watafiti.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na American Psychological Association’s ni kuwa zaidi ya 99% ya watu wazima humiliki simu za mikononi aina ya Smart phones na 74% wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram na Snapchat.

Wakielezea uhusiano uliopo kati ya mitandao ya kijamii na msongo wa mawazo Wanasayansi wanasema:>>>“Watu wengi hupata msongo wa mawazo kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii kwa kuangalia simu zao kila wakati, kutamani vitu ambavyo hawana kwa kuona kwa watu wanaowafollow katika mitandao na kupata hofu kubwa inayoweza kupelekea kupata msongo wa mawazo”

Source: Millard ayo