Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemuhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anayetuhumiwa kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kufuatia kauli yake ya kwamba wabunge wanasinzia Bungeni jambo lilotafsiriwa kudharau chombo hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka George Mkuchika amethibitisha kuhojiwa kwa RC Makonda na kuahidi kuiwasilisha ripoti kwa Spika wa Bunge Job Ndugai aliyewatuma kumuhoji.
 Source: Millard ayo