TATIZO LA HARUFU MBAYA MDOMONI NA TIBA YAKE.

TATIZO LA HARUFU MBAYA MDOMONI NA TIBA YAKE.

Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.

Zifuatazo ni baadhi tiba ambazo ni rahisi kuandaa mwenyewe ukiwa nyumbani na hazina madhara kabisa kiafya.

1. CHAI YA KIJANI (GREEN TEA)

Green tea ni tajiri wa polyphenol,ina antioxidant yenye nguvu sana ambayo itaondoa plaque kuenea kwenye meno yako. Polyphenols imeonekana kuzuia bacteria kukua katika mdomo.Kwahiyo kufyonza chai ya kijani husaidia kuondoa harufu chafu ya vitunguu. Spinach, chai ya rangi,apples na mushrooms pia nazo zina polyphenols, unaweza pia kutumia aina hii ya vyakula na kinywaji baada ya kujiona mdomo unatoa harufu iliosababishwa na mlo wako.

2. MATUNDA NA MBOGA FRESH

Fiber-nyingi hupatikana kwenye matunda na mboga, husaidia kuondoa harufu mbaya ya mdomoni (na kujisikia umeshiba muda wote,ambayo husaidia kupunguza uzito). Fiber kwenye vyakula vingi husaidia kutengeneza mate,ambayo husaidia kusafisha plaque zinazojijenga. Fiber imo kwenye vyakula kama cerely,apples,na karoti. Enzymes wa asili wanaptikana kwenye apples ,berries, nanasi, na kiwi huondoa sulfur compounds na huondoa harufu mbaya ya mdomoni.Mboga zenye vitamin C, kama red bell peppers na broccoli husaidia kutengeneza mazingira ya kuzuia bacteria wa mdomoni,pindi inapoliwa hufanya kazi hiyo.Hivi vyakula pia husaidia kuondoa mabaki ya vyakula katika meno pia.

3. MAZIWA

Kufyonza maziwa huondoa harufu mbaya ya mdomo KAMA utakunywa kabla au wakati wa kula (according to a Journal of Food Science 2010 study). Mafuta katika maziwa huyeyusha sulfur wakati maji kwenye maziwa huwa kama kisuuza mdomo. Siwezi kula maziwa bila cookies sa sijui hii inafanya kazi hapa.Kunywa maziwa baada ya kutumia chakula chenye viungo hii haisaidii kuondoa harufu mbaya.

4. MKATE

Kukosa carbs katika mlo wako huchangia harufu mbaya ya mdomo.Kula kipande cha mkate husiadia kuleta harufu nzuri mdomoni. Baada ya kula kipande cha kitunguu, kipande cha mkate kitasaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni,lakini ladha hubakia kwenye ulimi. Hata hivyo ukila kipande cha mkate huondoa hiyo harufu na utakua umehifadhi calories kwa matumizi mengine.

5. MITI SHAMBA FRESH

Kabla ya mouthwash hazijajulikana,watu walikuwa wakitafuna miti shamba kuondoa harufu mbaya. Miti shamba ina chlorophyll, ambayo huondoa harufu na uchafu.Aina ya mitishamba mizuri na fresh ni kama parsley, mint, binzari, basil, rosemary, thyme, tarragon na cilantro. Kama chakula chako kitakua na aina yoyote ya miti shamba tafuna kwa kuondoa harufu.Baada ya chakula pia unaweza tafuna yoyote ambayo unao uwezo wa kuipata na huondoa harufu mbaya mdomoni.

6. HARADALI(MUSTARD)

Kuna njia mbili tofauti zipo katika haradali (mustard). Kwanza,chukua kijiko cha chai cha haradali weka mdomoni, sukutua kisha tema kwa dakika chache. Kisha chukua nusu kijiko cha chai cha haradali meza itaenda tumboni ambapo itaenda kuua harufu ya vitunguu thoum na vitunguu mwilini. Njia ya pili ,kuchanganya vijiko vya chai viwili vya mafuta ya haradali na chumvi. Kisha weka mdomoni huku ukichezea ndani ya mdomo,tema mate yatayojitokeza na iache haradali kwa dakika 30 .

7. MAZIWA YA MTINDI

Ounches sita za maziwa ya mtindi husaidia kuondoa harufu mbaya na uchafu ambayo husababisha hydrogen sulfide na huua wadudu wa mdomoni. Tumia
kwa kunywa maziwa ya mtindi kila siku.

8. MBEGU & Kahawa (COFFEE BEANS)

Kutafuna karafuu, au hiliki, shamariand (fennel), mbegu za anise, mara moja huondoa harufu mbaya mdomoni.Kama unahisi unatatizo la aina ya vyakula kwa sababu ya meno, kuwa makini na hizi pia.Kula kahawa(coffee beans) ilo kaushwa ni nzuri zaidi na huondoa harufu mbaya.

9. NDIMU

Kulamba ndimu au kutafuna ganda dogo la ndimu ni nzuri kwa kuondoa harufu mdomoni pia.Lakini juisi ya ndimu ina acid na huweza kuwa mbaya kwa meno yako, husababisha meno kupata ganzi.

10. JUISI YA SIKI YA APPLE

Ni nzuri! Sio tu kwa ajili ya kusukutua ½ kijiko cha chai cha juisi ya siki ya apple iliochanganywa na kikombe cha maji,husaidia harufu pia,huondoa harufu ya vitunguu na huwa ni ladha pia ulimini.Kuchanganya na maji,huondoa ule ukali wake na utausikia mdomo uko vizuri mwepesi.Naifanyia kazi post zijazo kuhusu juisi ya siki ya apple na matumizi yake.

11. BAKING SODA

Kutengeneza mouthwashya baking soda na maji ni tiba ya asili ya muda mrefu. Tumia hii kwa kusukutua mara moja kwa siku.

12. MAJI

Pindi unywapo maji baada ya kula vitunguu au vitunguu thoum unaweza kuhisi haiondoi harufu na uchafu hapo hapo, kunywa maji mengi kwa mpangilio au utaratibu maalum husaidia mdomo kuwa fresh na harufu nzuri muda wote. Maji yanasaidia kuondoa bacteria wa kwenye chakula na huzidisha utengenezwaji wa mate kwa wingi, na pia huwa kama ni kiosha au kisafisha mdomo cha kudumu.

Harufu mbaya ya mdomo inakera ukiangalia vyakula vyenyewe hivi vya viungo na uzembe wa usafi unaoweza sababisha hata ukavu wa mdomo,vijidudu vya kwenye fizi, na vijidudu.Kama utagundua tatizo hili la harufu mdodmoni inaendelea,muone daktari wa meno kwa tiba na ushauri zaidi.

@moodyhamza