Msanii wa Kongo asikitika kuikosa Show ya Diamond Platnumz

Msanii wa mzuiki wa kizazi kipya na mmiliki wa Fizi Empire kutoka Kongo mwenye makazi yake nchini Uholanzi, Makiwa Chandja a.k.a King Fanatic ameonekana kuumia zaidi kutokana kuona kuwa atashindwa kuhudhuria show ya Staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz itakayofanyika tarehe 1 Julai mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Akizungumza na Dizzim Online kuhusu muziki wake, changamoto ya kufanya kazi ya muziki mbali na nchi yake na Maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambayo ndo maudhui ya show ya hiyo ya Diamond Platnumz, Fantic amesema kuwa alipoona mtadaoni kuwa Diamond Platnumz atakuwa nchini Kongo aliwaza kuhusu wapenda burudani ya muziki watakoudhuria ni kwa jinsi watakavyopata burudani ambayo asingependa kuikosa.

“Nilikuwa niko kwenye plan na maadalizi ya kuhudhuria show ya Diamond Platnumz itakayofanyika Kongo nyumbani na mimi nikaadhimishe miaka 57 ya uhuru wa nchi yangu, lakini kutokana shughuli za kikazi na kuwa busy imenibidi nisiweze kusafiri lakini nilikuwa na hamu ya kuona ni kitu kikubwa atakachofanya” Alisem King Fantic.

“show hiyo naamini itakuwa kubwa hivyo itatoa fursa kubwa za kibiashara kwasababu naamni watu watapata manufaa kwa kufanya biashara kupitia show hiyo na ukubwa wa siku hiyo” Aliongeza.

Hata hivyo msanii huyo baada ya kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Today Than Yesterday’ aliyomshirikisha mkali kutoka Burundi Big Fizzo, King Fantic anafanya vizuri na wimbo wake unaokwenda kwa jina ‘Rudi Afrika.’

Source: Dizzim online