Lil Wayne Ataka Kuifunga Label Ya Young Money.

Lil Wayne ametishia kuifunga label ya Young Money kama uendeshwaji wake usiporudi kwenye mstari. Rapper huyo anadaiwa kuwasilisha nyaraka za kisheria kutaka kuteuliwa kwa mtu atakayesimimia uendeshwaji wa label hiyo ama kuagiza kuvunjwa kwa mradi wa ushirikiano wa label ya Young Money. Ripoti imedai kuwa Brian “Birdman” Williams alijibu ombi hilo kwa kudai kuwa Wayne hana mamlaka ya kuivunja label wakati bado yupo chini ya Cash Money. Wayne na Birdman wamekuwa kwenye vita vya kisheria kwa muda sasa. January 2015, Wayne aliishtaki Cash Money na Birdman akitaka alipwe $51m. Source:Dizzim Online.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!