Swali alilouliza Mbwana Samatta kuhusu kuibadilisha jina Dar es Salaam

Mtanzania Mbwana Samatta tayari yupo Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kimataifa ya kirafiki iliyo katika kalenda ya FIFA ambapo Tanzania itachezwa jumamosi ya March 25 na March 28 ikianza na Botswana na baadae Burundi.

Samatta ambaye ndio nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars jioni ya March 22 2017 kupitia ukurasa wake wa twitter amejaribu kutoa wazo na kuuliza swali kwa watu wake kuwa “Nina wazo kwa nini Dar isibadirishwe jina ikaitwa Kolomije kwani tutapungikiwa nini  

Swali la Samatta limechukuliwa kama utani tu kutokana na jina la kijiji cha Kolomije kilichopo Mwanza kimekuwa maarufu kutokana na kutajwa mara kwa mara hivi karibuni katika mitandao ya kijamii.

Source: Millard ayo