Yanga wamepangwa na MC Alger wala hawaifikirii kwa sasa

Baada ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kuipanga Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria, tumempata katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa aelezeee maandalizi ya mchezo huo vipi anaifahaumu MC Alger?

“Ni vigumu kusema sasa hivi tumejiandaaje na mechi hiyo lakini timu imeanza mazoezi baada ya kurudi lakini sisi kwa sasa mechi ambayo tunaiangalia ni mechi dhidi ya Azam FC April 1 baada ya hapo ndio tutaanza maandalizi ya mechi ya MC Alger”

Source: Millard ayo