Msanii wa muziki wa RnB kutoka Tanzania, Ben Pol baada ya kuzungumzwa mengi kuhusu picha zake za nusu utupu huku maoni mengi yakiwa katika mitandao ya kijamii, amesema kuwa yuko tayari kurudi kufanya jambo la namla ile tena.
Akizungumza na Dizzim Online Ben Pol amesema kuwa sababu za kufanya vile zinamlinda kama msanii huku akibainisha kuwa hajutii kufanya jambo hilo la upigaji picha zilizotafsiriwa kuwa zenye kukiuka maadili na baadhi ya watu huku picha hizo mapema leo zikijibiwa kwa kuachia wimbo kutoka kwa Ben Pol unaokwenda kwa jina la ‘Tatu’ wimbo ambao maudhui yake ni utekwaji wa kimahaba zaidi.
Source: Dizzimonline