Usipokuwa na hela sahau kupata mapenzi ya dhati – Msami

Msami anaamini kuwa hakuna mapenzi ya dhati kwenye umaskini. Ameimbai Dizzim Online, kuwa hiyo ni sababu kubwa kwanini kwake mapenzi ameyapata nafasi ya tatu. Ya kwanza na ya pili ni nini?

“Nimekaa nikagundua kwamba kwenye maisha mapenzi ni watu wachache sana wanaoweza kumpenda mtu ambaye hana kitu kabisa. Na kama atakupenda wakati hauna kitu basi lazima atakuwa na mtu mwengine ambaye anampa anachokihitaji. So ukitaka kupata mapenzi ya dhati, lazima uwe na chanzo cha kipato na ndiyo maana mapenzi kwangu nimeyapa nafasi ya tatu, baada ya kumuomba Mungu nirudi kutafua pesa nimalizie na mapenzi,” amesema.

Msami aliwahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Irene Uwoya na Kajala.

Source: Dizzimonline