Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifikiri kufanya kazi na mtoto wa kike kuna vitu vingi sana hutokea, moja wapo kutokufikia malengo au kazi kutokufanyika kwa wakati. Lakini hii imekuwa tofauti kwa msanii wa R&B, Maua Sama ambaye yeye kazi zake za muziki zinasimamiwa na mwanamke.
Maua amesema anafurahi kufanya naye kazi na hakufikiria kama anaweza kuwa vile alivyo.
“Unajua nipo chini ya mwanamke kwa muda sasa na hakuna ugumu wowote kama wanavyofikiria. Pia amekuwa akinisaidia sana kiukweli. Maua wa sasa hivi tofauti na yule wa zamani vitu vingi vimebadilika kupitia yeye, so namshukuru sana meneja wangu,” ameimbia.
Msanii huyo aliongeza na kusema,” boss wangu ni mkali sana, huwaga hanaga mzaha linapokuja suala la kazi jambo hilo linanifanya nizidi kuamini uwepo wake na kuamini nitakuja kufika mbali zaidi ya hapa nilipo.
Source: Dizzimonline