Alichokisema mume wa Shamsa Ford baada ya kudaiwa kumpiga mke wake

U Heard ya April 25, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametusogezea stori kumhusu staa wa Bongo movie Shamsa Ford ambaye siku chache zilizopita alitoa taarifa za kupigwa na kupasuliwa sehemu ya jicho.

Shamsa Ford alidai kupigwa bila kukusudia wakati akiamulia ugomvi wa msichana wake wa kazi, lakini zipo taarifa zinasema majeraha hayo yametokana na kupigwa na mume wake Chidi Mapenzi baada ya kufumwa akinywa pombe.

Ili kuujua ukweli wa tukio hilo Soudy amepiga story na Chidi Mapenzi na haya ndiyo aliyoyasema:>>>”Siwezi kumpiga mke wangu. Wewe mwenyewe unanijua mimi siyo mgomvi. Nilitoka ofisini, nikamkuta mke wangu ameumia, nilipomuuliza nini tatizo, akanielezea. Nilipomuuliza unamjua mtu mwenyewe, akasema tumeyamaliza. Basi nikampeleka hospitali.” – Chidi Mapenzi.

Source: Millard ayo