Wanawake Huvutiwa zaidi na Wanaume wenye Sifa Hizi.

Utafiti mpya uliofanywa Australia umeonesha kuwa wanawake wengi huvutiwa zaidi na wanaume wenye tabia ya kula mboga za majani kwa wingi.

Timu ya Watafiti kutoka Macquarie University, Australia wamebaini katika Utafiti wao kuwa wanaume ambao hutumia mboga za majani na matunda kwa wingi huwa na rangi nzuri ya ngozi, hunukia vizuri na wanakuwa na afya nzuri zaidi kuliko wanaume wanaokula vyakula vya wanga kwa wingi.

Watafiti hao pia wamebainisha kuwa wanaume ambao wanapenda kula nyama kwa wingi miili yao hutengezeka harufu nzito ambayo haijabainishwa kuwa ni nzuri au mbaya wakati wale wanaopenda kula vyakula vizito vya wanga hutoa harufu isiyo nzuri.

Source: Millard ayo