Kutana na Jackline N. Mengi, Mwanamke mwingine wa Tanzania ambaye juhudi zake zinaanza kumnyanyua kumpeleka kwenye headlines za dunia huku zamu hii ikiwa ni Dubai kupitia kampuni yake ya kutengeneza FURNITURE.
Kabla ya kuendelea kuisoma hii taarifa ni vyema ukatambua kwamba kwa ubunifu wake wa kutengeneza Furniture umempa ushindi wa tuzo mbili huko Italia, moja ikitokana na kiti na nyingine kutoka kwenye bidhaa zake za Taa.
Amesema ‘Tangu nifungie brand ya MOLOCAHO watu wameipokea vizuri nje na ndani ya Tanzania, hii ya sasa hivi Dubai ni kuonyesha bidhaa zetu kwenye maonyesho ambayo yatajumuisha Makampuni mengine 800 duniani”
‘Ni maonyesho ya kila mwaka ya Dubai ( kama sabasaba) na ni nafasi nzuri kwa MOLOCAHO kujulikana kimataifa na kupanua wigo wetu wa kibiashara na pia kuonyesha Tanzania tunaweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kimataifa zinazoweza kutumika popote duniani‘ – Jackline
‘Wakati nakua nilikua najua kabisa ningependa kuwa Msanii (Artist), nilikua napenda kuchora.. kuimba… nilikua napendelea vitu vyote ambavyo vinahusisha ubunifu zaidi kwahiyo ku-design furniture haijatoka mbali na ndoto yangu ya utotoni, toleo la kwanza la MOLOCAHO vitu vyote nime-design na kuchora mwenyewe ‘ – Jackline
‘Niko Inspired na Wafanyabiashara mbalimbali mfano Mume wangu ambaye amefanikiwa sana katika biashara ni mmoja wapo wa Inspiration yangu kubwa sana, nikimuangalia alikotoka na sehemu alipofika inanipa moyo kwamba chochote nikikifanya vizuri naweza kufanikiwa sana‘ – Jackline N. Mengi
Jackline N. Mengi ambaye ni Miss Tanzania 2000 alizindua rasmi bidhaa zake za FURNITURE September 2016 ambapo mbao ya mninga kutoka hapahapa Tanzania ndio anayoitumia kutengeneza viti, sofa, meza na bidhaa nyingine…
Source: Millard ayo