Ni nini maana ya Uislamu?

Maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumpwekesha na kufuata maamrisho yake kwa utii na kuepukana na shirki kama Allaah Anavyosema:

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyeuelekeza uso wake kwa Allaah naye ni mtendaji mema na akafuata Dini ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki). Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni khaliyl (kipenzi).[1]

 

Anasema pia:

 

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗوَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

Na anayesilimisha uso wake kwa Allaah, naye ni mtenda wema, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni mwisho wa mambo (yote).[2]

 

Na Anasema pia:

 

فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤

Basi Ilaahu[3] wenu ni Ilaahun Waahid (Mungu Mmoja Pekee); basi kwake Pekee jisalimisheni. Na wabashirie wanyenyekevu.[4]



[1] An-Nisaa (4: 125)

[2] Luqmaan (31: 22)

[3] Mungu Anayestahiki kuabudiwa kwa haki.

[4] Al-Hajj (22: 34)

story@moodyhamza