Sean Kingston amaliza utata wa kuishiwa kifedha.

Staa wa muziki kutoka Marekani mwenye asili ya nchini Jamaika, Kisean Anderson a.k.a Sean Kingston amekanusha uwepo wa taarifa za kuwa ameishiwa kifedha baada ya kusambaa kwa taarifa ya mahakama kutoa amri ya kuwa akamatwe kwakuwa ameshindwa kumlipa maelfu ya Dola kadhaa za mfanya biashara muuza vidani vya thamani huko Miami.

Kingston katika hili imeendelea kuzungumziwa zaidi kuwa ameishiwa katika hali hiyo ya kudaiwa deni kwakuwa aliendelea kupost picha za umiliki wake wa vitu vya kifahari kama gari na nyumba. Kingston katika video ya hivi karibuni amesikika kakiukataa uvumi na maneno ya kuwa ameishiwa ambapo alithibitisha kuwa bado namiliki mkwanja mrefu kwakuwa haiwezekani awaandikie muziki mastaa kama Chris Brown na Justin Bieber na bado akawa ameishiwa.

“Yo can write songs for Chris Brown and Justin Bieber and them man there and broke, a what happen to some man, stop believe everything yo hear,” katika video alisikika Kingston.

Hata hivyo ukizungumzia muziki na umaarufu wa Kingston kibiashara utagundua kuwa yupo katika ushirikiano na kampuni ya headphones ya Beats By Dr. Dre ambapo ameweza kuzindua bidhaa yake ya Headphones pia zinazofahamiuka kwa jina la Monster Box.

Kupitia Moster Box, Kingston anayemiliki utajiri wa dola milioni 2 ana uhakika wa kupata asilimia 12 ya mauzo na habari njema nyingijne ni kuwa karibuni anakuja na kipindi cha runinga kitakacho zungumzia maisha yake ya ndani zaidi na kitapatikana kwa watazamaji kupitia kituo cha E.

Source: Dizzim Online.