Mtanzania aliyekataa kazi ya millioni moja marekani asema

Huwa yanatajwa kuwa maamuzi magumu pale ambapo unashawishika kuacha kazi inayokupa mshahara wa uhakika kila mwezi alafu uende kuanzisha biashara yako binafsi ambayo hata hivyo huna uhakika kama itakulipa kufikia mshahara uliouacha.

Hiyo ilitokea kwa Upendo Shuma ambaye ni maarufu kwa sasa kupitia Lavie Makeup ikiwa ni kibarua chake binafsi cha kupamba Maharusi na watu wengine mbalimbali ambapo jarida la FORBES lilipofahamu kuhusu biashara yake, baada ya uchunguzi likabaini kuwa kwa anachokifanya… huyu ni Milionea Mtarajiwa.

Upendo ni kama Watanzania wengine ambao walikaa nyumbani kwa miezi sio chini ya nane wakisubiri kupata kazi ya mshahara mzuri baada ya kumaliza chuo ambapo baada ya kupita huku na huku akapata kazi iliyokua inampa mshahara wa zaidi ya milioni moja kwa mwezi kwenye shirika la ndege.

Kwa mshahara huo mwingine angeweza ku-relax lakini yeye alisema hapana, akafanya kazi kwa muda na kuamua kuacha ili afanye biashara binafsi kitu ambacho hakikuungwa mkono na baadhi ya wanaomzunguka sababu waliona ni kama anachezea bahati.

Alisimama kwa ujasiri kusema hata kama akianguka, atakua ameuridhisha moyo wake kufanya kile ulichomsukuma………….. baada ya kukomaa hatimae leo hii jarida la FORBES limemuweka kwenye orodha ya Vijana Mamilionea Watarajiwa Afrika,

Source: Millard ayo