Ronaldo kupanda Mahakamani Hispania.

Cristiano Ronaldo yupo nchini Hispania ambako atafika mahakani siku ya Leo Jumatatu kusikiliza kesi yake inayomkabili ya ukwepaji wa kodi.

Ronaldo, 32 ambaye ni Mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi Duniani anashitakiwa kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya Paundi Milioni 13.1 tangu Mwaka 2010.

Sakata la ukwepaji wa kodi kwa Wachezaji wa nchini Hispania linazidi kuwa kubwa, Nyota kadhaa wamewai kukutwa na hatia hiyo akiwemo Angel Di Maria, Luca Modric pamoja na nyota wa Barcelona Lionel Messi aliyekutwa na hatia ya kukwepa kodi ya Euro Milioni 4.1 ambaye Mahakama iliamuru alipe faini ya uro 252,000 kama fidia ya kutotumikia kifungo cha Jela cha Miezi 12.

Kama Ronaldo atakutwa na hatia siku ya leo, Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Ureno anaweza kukumbana na adhabu ya kulipa Faini ya angalau Euro milioni 28 pamoja na kifungo cha Miaka Mitatu kwa mujibu wa sheria ambayo imeripotiwa na BBC.

Source: Dizzim online