Polisi jijini Nairobi inamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumpiga mke wake na mtoto wake wa kiume kwa madai ya matumizi mabaya unga wa ugali.
Mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika anadaiwa kuwapiga wawili hao akiwalalamikia kutumia vibaya fedha anazotoa kwa ajili ya matumizi.
Mtuhumiwa huyo amedai kuwa fedha hizo kidogo ambazo anapata shida mkewe na mtoto wamekuwa wakizitumia vibaya kununua unga wa ugali ambao gharama yake imepanda.
Inadaiwa kuwa baada ya kuwapiga alijisalimisha polisi huku mkewe na mwanae wakikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Source: Udaku