Dillish Mathews Ni Mjamzito?

Mshindi wa shindano la Big Brother Afrika mwaka 2013 kutoka nchini Namibia, Dillish Mathews huenda akawa ni mjamzito. Hii ni kutokana na picha aliyoweka Instagram jioni hii ikimuonesha akiwa ameshika tumbo lake na kuandika, “A baby or a burger?”

Picha hiyo imesababisha mjadala mkubwa kwa mashabiki wa Tanzania na sehemu zingine Afrika wanaolitaja jina la Diamond Platnumz kwenye comments kuwa kama kweli mrembo huyo ni mjamzito basi ni ya Chibudenga.

Hii ni kwasababu wiki tatu zilizopita, kulikuwepo na tetesi kuwa wawili hao walionekana pamoja Zanzibar na kwamba ni wapenzi. Diamond alikanusha tetesi hizo Jumanne iliyopita.

Shabiki mmoja ameandika: @zarithebosslady @diamondplatnumz theres number 2 outchea 😂.”

Mwingine ameandika: Diamond platinumz is the man going around the Africa giving women his babies 👶 congrats.”

“😂😂😂😂😂😂Yan km ni mimba naomba iwe ya chibude haki bibi tukinao atakufa…alafu ufanye uje madale sawa…km hujui kiswahili naomba tuu ujifunze😅😅😅😅,” ameandika mwingine.

Source: Dizzim Online.