Diamond aendelea kuwateka mastaa wa Marekani.

Milango ya kuwateka mastaa wa Marekani inaendelea kufunguka kwa Diamond. Baada ya Dj Khaled kumfollow na rapper Rick Ross kumpost hitmaker huyo wa Eneka kwenye mtandao wa Instagram, Swizz Beatz na yeye ameamua kufuata nyayo kama hizo.

 

Swizz ameonekana katika kipande ha video akimtaja Diamond. Hata hivyo haikuishia hapo producer huyo ambaye pia ni mume wa msanii Alicia Keys ame-comment katika video hiyo ambayo Diamond ameipost katika mtandao huo.

“@diamondplatnumz Bless up King😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂,” ameandika Beatz katika video hiyo.

Pia kwenye event aliyoiandaa Swizz Beatz ambaye amekuwa akitoa support kubwa kwa wasanii wa Afrika alipiga ‘Seduce Me’ ya Alikiba na ‘kisela’ ya Vanessa Mdee.

Source: TeamTz.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!