Beka Flavour Achukizwa Kufananishwa Na Aslay.

Msanii huyo amesema watu wanakosea sana kufanya hivyo ingawa ki kawaida huwezi kumzuia mtu kufanya kitu chochote.

“Mimi sioni sababu ya watu kutushindanisha kwasababu yeye anafanya muziki tofauti na mimi,” amesema Beka. “Sasa wanapofanya hivyo wanakuwa wanatukosea sana na hii sio kwetu tu tunaona hata kwa wasanii wengine wanafanyiwa hivyo. Tunaona kwenye mitandao ya kijamii, so mimi ninachowaomba wasupport muziki mzuri wangu na anaofanya Aslay. Lakini sio poa kutushindanisha, mimi binafsi sipendi na nachukizwa kila ninapoona hivyo,” ameongeza msanii huyo.

Mpaka sasa Beka anamiliki ngoma mbili zinazofanya vizuri mtaani huku Aslay naye akifanya vizuri kwa ngoma zake mpya zaidi ya nne alizoachia mwaka huu.

Source: DizzimOline.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors