baadhi ya fadhila za subira katika Qur-aan:

Subira imetajwa katika Qur-aan mara nyingi mno kama walivyonukuu Maulamaa. Wengine wamesema kwamba imetajwa zaidi ya mara themanini kwa kusifiwa wale wenye kuvumilia mitihani inayowasibu. Ama kwa ujumla, subira imetajwa katika Qur-aan zaidi ya mara mia.

 

Zifuatazo ni baadhi ya fadhila za subira katika Qur-aan:

 

1.       Wenye kusubiri hupata mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

((وَاللّهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ))

((…na Allaah Anawapenda wanaosubiri)) [Aal-‘Imraan: 146]

 

 

2.       Allaah (سبحانه وتعالى) Yu pamoja nao daima:

 

((إِنَّ اللّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ))

((….hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri)) [Al-Anfaal: 46]

 

 

3.       Allaah (سبحانه وتعالى) Amewajumuishia mambo matatu ya bishara njema; Baraka [na maghfirah], Rehma Yake (سبحانه وتعالى), na uongofu.

((وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوفْ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الأَمَوَالِ وَالأنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ

الصَّابِرِينَ )) ((الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ))  ((أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ

صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ))

((Hapana shaka Tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanaosubiri)) ((Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Allaah, na Kwake Yeye hakika tutarejea)) ((Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na Rehma, Nao ndio wenye kuongoka))  [Al-Baqarah: 155-157]

 

 

4.       Allaah (سبحانه وتعالى) Ameahidi kuwalipa malipo mazuri kabisa kwa sababu ya kusubiri kwao katika utiifu.

((وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُواْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ))

 

((Na bila shaka Tutawalipa ambao wamesubiri ujira wao kwa mazuri waliyokuwa wakitenda)) [An-Nahl: 96]

 

 

5.       Wenye kusubiri wameahidiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) malipo mema yasiyohesabika.

 

(( إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ))

 

((… Na bila shaka wafanyao subira watalipwa ujira wao pasipo hesabu)) [Az-Zumar: 10]

 

 

6.       Allaah (سبحانه وتعالى) Ameambatanisha subira na mafanikio na Amewaahidi kufuzu.

 

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ))

 

((Enyi mloamini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni imara, na mcheni Allaah ili mpate kufaulu)) [Aal-‘Imraan: 200]

 

((إِنِّي جَزَيْتُهُمْ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمْ الْفَائِزُونَ))

 

((Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyosubiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu)) [Al-Muuminuwn: 111]

 

 

7.       Allaah (سبحانه وتعالى) Amewasifu kuwa ni miongoni mwa wakweli waliosadikisha na wenye taqwa.

 

 ((وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاء والضَّرَّاء وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ))

((…na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita, hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wenye taqwa)) [Al-Baqarah: 177].

 

 

8.        Allaah (سبحانه وتعالى) Ameahidi maghfirah na ujira mkubwa kwa wenye kusubiri na wakatenda mema.

 

 ((إِلاَّ الَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ أُوْلَئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ))

 

((Isipokuwa ambao wamevumilia wakatenda mema, hao watapata maghfirah na ujira mkubwa)) [Huwd: 11]

 

 

9.       Wanaovumilia wamehusishwa na uongozi wa Dini na kuwa ni wenye yakini kuhusu yaliyoteremshwa kwao na Mola wao.

((وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ))

 

((Na Tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoa watu kwa amri Yetu, waliposubiri na wakawa na yakini na Ishara Zetu)) [As-Sajdah: 24]

 

 

10.     Allaah (سبحانه وتعالى) Ameifanya subira kuwa ni kinga kubwa kwa maadui na hila zao kama walivyoaahidiwa Maswahaba katika vita vya Uhud.

 

 ((وَإِن تَصْبِرُواْ وَتَتَّقُواْ لاَ يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا إِنَّ اللّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ))

((Na mkisubiri mkawa na taqwa hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Allaah Anayajua vizuri yote wanayoyatenda)) [Aal-‘Imraan: 120]

 

 

11.     Allaah (سبحانه وتعالى) Ameifanya kuwa ni jambo la kutakwa msaada pamoja na nguzo ya Swalah na kuwasifu kuwa wenye kuvumilia ni wenye sifa ya unyenyekevu.

 

((وَاسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاَّ عَلَى الْخَاشِعِينَ))

 

((Na jisaidieni kwa kusubiri na kwa kuswali, na hakika jambo hilo ni gumu ispokuwa kwa wanyenyekevu)) [Al-Baqarah: 45]

 

 

12.  Allaah (سبحانه وتعالى) Amewasifu wenye kuvumilia misiba, maudhi na dhulma kwamba hilo ni jambo kuu la kuazimiwa.

 

((وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الأُمُورِ))

 

((Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa)) [Ash-Shuwraa: 43]

 

 

13.     Wenye kuvumilia bila shaka watapewa kheri nyingi na wenye hadhi kubwa.

 

(( وَمَا يُلَقَّاهَا إِلاَّ الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إلاَّ ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ))

((…lakini hawapewi wema huu ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye hadhi kubwa)) [Fusswilat: 35]

 

 

14.     Allaah (سبحانه وتعالى) Ameambatanisha ushindi kwa subira na taqwa.

 

(( بَلَى  إِن تَصْبِرُواْ  وَتَتَّقُواْ  وَيَأْتُوكُم  مِّن فَوْرِهِمْ  هَذَا  يُمْدِدْكُمْ  رَبُّكُم  بِخَمْسَةِ  آلافٍ

 مِّنَ الْمَلآئِكَةِ مُسَوِّمِينَ))

((Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkawa na taqwa na hata maadui     wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wanaoshambulia kwa nguvu)) [Aal-‘Imraan: 125]

 

 

15.     Allaah (سبحانه وتعالى) Amesifu kila ambaye ananufaika na Aayah Zake na akaathirika na mawaidha kwamba ni mwingi wa kusubiri na kushukuru:

 

((إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ))

 

((Hakika katika hayo ni ishara kwa kila mwingi wa kusubiri, mwingi wa kushukuru)) [Ash-Shuwraa: 33]

 

16.     Amemsifu Nabii Ayyuub (‘Alayhis Salaam) kwa subira yake kuwa ni mja mzuri alioje.

(( إِنَّا وَجَدْنَاهُ صَابِرًا نِعْمَ الْعَبْدُ إِنَّهُ أَوَّابٌ))

 

((Hakika Tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu)) [Swad: 44]

 

 

17.     Allaah (سبحانه وتعالى) Amehukumu

kukhasirika kwa binaadamu pindi asipokuwa miongoni mwa wenye kuusia subira na akavumilia  mwenyewe pia:

 

((وَالْعَصْرِ)) ((إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ))((إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا

 بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْر ))

((Naapa kwa Zama!)) ((Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara)) ((Ila wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri)) [Suratul-‘Aswr]

 

 

18.     Allaah (سبحانه وتعالى) Amewahusisha watu wa kuliani ambao ni watu wa kheri kwamba ni watu wenye subira wenye huruma.

 

((ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ )) ((أُوْلَئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ))

 

((Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana)) ((Hao ndio watu wa kheri wa kuliani)) [Al-Balad: 17-18]

 

 

19.     Hatimaye Akhera ambako ndio kwenye maisha ya kudumu na milele wameahidiwa Pepo na Neema zake:

 

((وَجَزَاهُمْ بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا))

((Na Akawalipa Mabustani ya Pepo na [nguo za] hariri kwa sababu ya kusubiri kwao))   [Al-Insaan: 12]

 

 

20.     Na pia watabashiriwa Pepo na neema zake na amani kutoka kwa Malaika.

((جَنَّاتُ  عَدْنٍ  يَدْخُلُونَهَا  وَمَنْ صَلَحَ  مِنْ آبَائِهِمْ  وَأَزْوَاجِهِمْ  وَذُرِّيَّاتِهِمْ  وَالمَلاَئِكَةُ  يَدْخُلُونَ

 عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ)) ((سَلاَمٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ))

 

((Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na waliowema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawajia katika kila mlango)) [Wakiwaambia] Assalaamu ‘Alaykum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Aakhirah)) [Ar-Ra’d: 23-24]

 

Lakini si wepesi kuipata, na miongoni mwa watakaiopata ni waja waliosubiri katika kufanya Jihaad katika njia ya Allaah (سبحانه وتعالى) ambayo wamekumbwa na mateso mbali mbali. Allaah (سبحانه وتعالى) Amewatia mtihanini ili Awatambue kama walivumilia kweli:

 

((أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللّهُ الَّذِينَ جَاهَدُواْ مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ))

 

((Je! Mnadhani mtaingia Peponi na hali Allaah Hajawapambanua wale miongoni mwenu waliopigana Jihaad, na Hajawapambanua waliosubiri?)) [Aal-‘Imraan: 142]

story@moodyhamza