Msanii Alikiba Amwagia Sifa Aslay.


Msanii Alikiba ambaye hivi sasa anaendelea kufanya vyema na wimbo wake ‘Seduce me’ amefunguka ya moyoni na kumpa sifa msanii ambaye alikuwa anaunda kundi la Yamoto Band, Aslay na kusema kuwa anajua sana.

Alikiba amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati na kusema msanii huyo anaweza pale aliposikiliza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Natamba’ ambayo imetoka siku mbili zilizopita na kuendelea kufanya vyema na kupokea vizuri na mashabiki.
Ngoma hiyo ya Aslay ‘Natamba’ ni kati ya ngoma kumi na tisa ambazo ameachia nyota huyo toka ameanza kufanya kazi kama ‘Solo Artist’ nyimbo ambazo zimeweza kumpatia mashabiki wengi zaidi nchini na kufanya kazi zake kuendelea kupendwa zaidi kutokana na tungo zake.

Source: Udaku.