Tekno hakuwa akinijua.

Rais wa Manzese, Madee amesema Tekno hakuwa akimjua wakati wanamuomba afanye naye collabo. Akipiga story na Dizzim Online, Madee amesema Tekno hakuwahi kulisikia jina lake hata siku moja.

“Kwa mara ya kwanza Tekno anaambiwa na Babutale, kiukweli alikuwa hafahamu huyo Madee ni nani. Lakini yeye alikuwa anamuamini ni Babutale, anamuamini sana kwasababu anaona ni meneja mkubwa anameneji wasanii tofauti tofauti akiwemo Diamond, so akajua mimi siwezi kuwa msanii mbaya,” amesema Madee.

“So akaanza kupitia kazi zangu, akaangaliA baadhi ya show zangu pia akaona it’s okay, lakini akaomba beat atengeneze yeye mwenyewe, tukamkubalia akafanya hivyo na mwisho wa siku kazi ikaachiwa hewani.”

Wimbo huo ambao Madee amemshirikisha Tekno unaitwa Sikila ambao video yake ni ya katuni.

Source: Dizzim online