Lavalava Aongea Na Mashabiki Wake.

Msanii wa label ya WCB, Lavalava ametuelezea vigezo ambavyo alivitumia kumchukua model aliyetumika kwenye video ya wimbo wake mpya, Dede.

Amesema kuwa hakutaka kutumia mrembo mwenye uzuri wa kupitiliza.

“Mara ya kwanza wakati tunaanza kutafuta video queen tulikuwa tunawaza mwanamke mzuri sana ambaye anastahili kupewa hilo jina la Dede. Lakini baada ya kujadili sana tukaona sio watu wote au sio wanaume wote wana wanawake wazuri kila mtu ana mwanamke na unaweza kukuta kuna mwanaume ana mwanamke ambae hana mvuto mbele za watu lakini kwake yeye akawa ni mzuri, so tukatafuta mwanamke ambae yupo pande zote yaani sio mzuri sana na wala sio mbaya sana ili hata yule ambaye yupo kawaida anastahili kuitwa Dede,” amesema.

Source: Dizzim online.