Sare: 1-1 ya Man City vs Liverpool katika uwanja wa Etihad March 19 2017

Michezo ya Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 uliendelea leo March 19 2017 katika viwanja tofauti tofauti, moja kati ya michezo iliyochezwa Jumapili ya March 19 ni game kati ya Man City dhidi ya Liverpool, Liverpool safari hii wamesafiri hadi jini la Manchester kucheza dhidi ya Man City.

Liverpool ambao wapo nafasi ya nne katika msimamo wa EPL wamejikuta wakiambulia point moja dhidi ya Man City ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa EPL unaoongozwa na Chelsea kwa kuwa na point 69 tofauti ya point 10 na Tottenham Hotspurs waliyopo nafasi ya pili.

Licha ya kuwa ugenini Liverpool walianza kupata goli la kwanza dakika ya 51 kwa mkwaju wa penati uliyopigwa na James Milner lakini Man City ambao walikuwa wakiutawala mchezo kwa asilimia 59 kwa 41 dhidi ya Liverpool walifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 68 kupitia Sergio Aguero na game kumalizika na sare ya 1-1.