Baraka da Prince ambaye ameachia audio na video mpya ya wimbo wake wa “Acha niende” amefunguka ugumu aliokumbana nao kipindi hiki alipohojiwa na Harakati za Bongo
“Changamoto kubwa ni watu wanaconcertrate sana kwenye mambo yanaoyendelea kwenye ma’social network kuhusu serikali, sasa kuna mashabiki wetu wanakua wanapoteza muda wao mwingi huko, lakini mimi naamini sana kazi yangu na nyimbo nzuri inadumu” Baraka alifunguka.
Aidha Baraka amesema mambo yanayoendelea yanapita na kazi nzuri inadumu kwahiyo hana hofu na kazi yake.
Source: Teen tz