Rais Magufuli amualika Nay wa Mitego Ikulu Ijumaa hii


Rais Magufuli amemualika Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego Ikulu siku ya Ijumaa wiki hii.

Nay amepata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu Jumapili.

“Yeah ni kweli jana nilipa mwaliko lakini nimeambiwa niende Ijumaa kwa sababu kuna ugeni unakuja kwahiyo na mimi nimealikwa kuhudhuria,

Rapa huyo amedai bado nafikiria nini cha kuongea na Rais endapo atapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye.

Nay alikamatwa na polisi Jumapili iliyopita mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.

Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.

Source: Teentz