Kundi La Weusi Latoa Ya Moyoni


Joh Makini amesema hakuna mpango kwa sasa wa kuongeza members kwenye kundi lao la Weusi ambalo ni kampuni pia  Joh amesema kuwa watakaribisha watu kama wakiwa na uwezo wa ziada.

“Suala la kuongeza mtu kwa Weusi ni suala kidogo tofauti kwa sababu sisi sio kama kundi la muziki, sisi ni kampuni, kwahiyo sisi tunashare hisa na milango ipo wazi kufanya biashara na mtu yoyote mwenye idea au wanataka kuchangia mtaji labda halafu faida tunagawana, sio kuongeza mtu kama kuongeza mtu Weusi suala hilo hatuna,” amesema.

Aidha hakuacha kutaja vigezo wanavyoviangalia mpaka kuweza kushare na wao. “Sisi tunaangalia wewe una kitu gani cha kutuongezea sisi kipato ambacho sisi hatuna, yaani we una kitu gani kinachomiss kwenye biashara yetu na unamchango gani ili tuweze kupata faida zaida,” amesisitiza rapper huyo.

Source: Dizzimonline