Zawadi ya Ben Pol, Baraka Da Prince na Jux kwa Dodoma

March 3 2017 mastaa wa Bongofleva Juma Jux, Barakah Da Prince na Ben Pol wameandaa show kwa watu wao Dodoma ambayo itakuwa ni Live show mwanzo mwisho yaani bila kutumia CD na itafanyika Royal Village huku wakiwa wameipa jina la ‘333 Experience‘ huku MC wakiwa ni B dozen na MC Pilipili.

Sasa good news ni kwamba mastaa hao wameamua kushow love kwa wasanii chipukizi kutoka Dodoma ambapo kazi ni moja tu wasanii watashindanishwa kuimba na yule atakayeibuka mshindi atapewa shavu la kurekodiwa ngoma zake bure huku kazi yote ya usimamizi ikiwa kwao.

Yapo mengi wameyazungumza mbele ya waandishi wa habari Dodoma leo na tayari full video nimekuwekea hapa chini mtu wangu….