Rapa Dj Khaleed Aja Na Album Mpya.

Rapa mfanyabiashara ‘Dj Khaled’ katika kumshirikisha mwanae ‘Asahd Tuck Khaled’ kuandaa album ya ‘Grateful’ iliyoingia rasmi sokoni Juni 23 mwaka huu, taarifa rasmi zinasema kuwa tayari album imefika rekodi ya mauzo ya nakala milioni moja ‘Platnum’.

Khaled kupitia ukurasa wake wa Instagram alithibitisha kuwa Album yake hiyo imefikia rekodi hiyo ya mauzo na kingine cha tofauti imeonekana katika mtiririko wa matukio huku namba 23 kuonekana kuwa namnba ya bahati na ya kipekee katika hatua zote za kutoka na kufikia kiwango hicho cha mfanikio.

Ikiwa kama Album iliyosubiriwa na mashabiki kwa muda kutoka kwa Khaled tarehe rasmi ya kutoka kwa album hiyo ilitangazwa, June 23 ikatoka rasmi na kwa mujibu wa kumbukumbu ni kwamba tarehe 23 ya Mwezi Octoba mwaka jana Asahd Khaled alizaliwa na tarehe 23 ya mwezi August(Jana) Album hiyo ya ‘Grateful’ imegonga rekodi ya mauzo ya Platnum siku ambayo inahesabika kuwa Asahd ametimiza umri wa miezi 9.

Source: Dizzim Online