Forbes imewataja ‘Vijana 7’ wa kuwaangalia mwaka 2017, Watanzania ni wawili

Ni kazi ya millardayo kuhakikisha haupitwi na chochote, nakusogezea hii nyingine kutoka jarida maarufu linalofatilia taarifa za watu mashuhuri na vitu vya kushangaza duniani, FORBES limetoa list ya ‘Vijana 7 Wajasiriamali’ wa kuwaangalia zaidi mwaka 2017 wakiwemo Watanzania Jacqueline N. Mengi na Patrick E. Ngowi.

Vijana hao 7 waliotajwa kutokea Afrika wote wako chini ya miaka 40 na wamekuwa wakiwekeza nguvu na mali kwenye biashara ambazo ni za kipekee na ambazo zinakuwa kwa haraka zaidi barani Afrika na duniani.

Nimekuwekea hapa list nzima.

  1. Adeniyi Makanjuola – Nigeria
  2. Jacqueline Ntuyabaliwe – Tanzania
  3. Patrick E. Ngowi – Tanzania
  4. Ndijeka Akunyuli Crosby – Nigeria
  5. Fatoumata Ba – Ivory Coast
  6. Rupert Ryan – Afrka Kusini
  7. Ludwick Marishane – Afrika Kusini