Bill Nas Amkana Nandi.

Rapa Bill Nas ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya wa ‘Sina Jambo’ amefunguka kwa kumtolea nje Nandy kwa kudai hajawahi kutoka naye kimapenzi kama watu wanavyofikilia katika vichwa vyao kila kukicha.

Bill Nas ameeleza baada ya yeye kuhusishwa katika suala la kimapenzi na msanii wa bongo fleva Nandy na kusema hilo jambo halina ukweli wowote hata watu wake wa karibu wanashangaa kusikia hilo jambo.

“Siyo kweli, sijawahi kuhusiana na msanii yoyote wa kike iwe wa bongo fleva au bongo ‘movie’. Mtu wangu wa mwisho niliyekuwa naye alikuwa ameajiriwa katika kampuni binafsi. Mimi nipo ‘single’ hata watu wangu wa karibu wanaelewa hilo halafu hizo stoti mimi nazisikia kutoka kwa watu wa mbali “, alisema Bill Nas.

Pamoja na hayo, Bill Nas amesema kwa upande wake suala la mapenzi hawezi kulipa kipaumbele kama watu wengine wanavyofanya kwa madai linampoteza ‘focus’ katika vile alivyovipanga kuvitekeleza katika maisha yake.

Source: Udaku