Adhabu zilizotolewa na UEFA leo kwa Dele Alli wa Spurs, Arsenal na Bayern

Shirkisho la soka barani Ulaya UEFA leo March 24 2017 limetangaza adhabu kwa timu ya Arsenal, Bayern na kiungo wa Tottenham Hotspurs Dele Alli, UEFA imetangaza kuipiga faini Arsenal na Bayern huku Dele Ali akifungiwa mechi tatu za ngazi ya club.

Arsenal wamepigwa faini ya pound 4300 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 11.9 kutokana na kitendo cha mashabiki wake kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa marudiano wa UEFA Champions League dhidi ya FC Bayern Munich uliyochezwa katika uwanja wa Emirates na Arsenal kufungwa goli 5-1.

Huku kiungo wa Tottenham Hotspurs Dele Alli akifungiwa mechi tatu kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya KAA Gent mwezi uliyopita lakini FC Bayern Munich pia ilipigwa faini ya pound 2600 kwa mashabiki wake kurusha vitu uwanjani.

Source:Millard ayo