Kupitia 5 Selekt ya EATV, Baraka amesema kwanza ieleweke kuwa Naj ni mchumba wake na si mke, kwani mke ni neno zito na maana yake tayari mmefunga ndoa.
Jambo la pili ni kuhusu picha aliyowahi kuposti instagram kuhashiria Naj ni mjamzito, Barakah amefafanua kuwa, “kwanza kabisa picha niliyoiposti ilionesha Naj kanenepa, si maana kwamba alikuwa na mimba.
Ameongeza kuwa, “maana ya kuandika caption thanks God sio maana kwamba ana mimba, ujue hata mpenzi wako mwili wake ukibadilika unashukuru”.
Kitu kingine kuhusu Naj, amedai kwa siku huwa anachati nae mara kibao, “suala la kuchati na Naj ni mara nyingi sana, hapa hata dakika tatu nyuma nimetoka kumtumia message, nawasiliana nae mara kwa mara”.
Jambo la nne Barakah ameeleza siku anapewa tetesi kuwa Naj yupo sehemu fulani anachepuka, ni kitu ambacho hawezi kukiamini kwanza, na pengine itakuwa ni siku ya wajinga duniani.
Source: Udaku